Cha kwao ni chama cha maisha yaliyowekwa wakfu kwa Mungu kwa njia ya ahadi
ya kushika mashauri ya Kiinjili ya useja mtakatifu, ufukara na utiifu
kadiri ya utamadunisho safi wa karama ya udugu na udogo waliyorithi kwa
mtakatifu Fransisko wa Asizi. Mtindo wa maisha yao unakusudiwa kumfuata Yesu kwa kutekeleza kijumuia
Injili yake na kushikamana na watu wa leo walio fukara zaidi ili uwe
habari njema kwao na kwa wale wote wanaotamani dunia ijae haki, amani na
upendo. Wakiamini kwamba hiyo itabaki ndoto ya mchana tu ikiwa wanaume na wanawake
watajaribu kuujenga kwa nguvu zao wenyewe, Ndugu Wadogo wa Afrika
wanaikimbilia sala usiku na mchana kusudi uhusiano na maongezi na Baba wa
wote vizijalie akili furaha ya ukweli, viunganishe mioyo, vitakase na
kuimarisha ndani ya kila mmoja nia ya kutumikia kwa ukarimu wenye shida
kubwa zaidi na viwafanye wote kuwa vyombo vya amani yake. Roho Mtakatifu, tunayeshirikishwa kwa njia ya Yesu mteswa, mzikwa na mfufuka,
ndiye anayegeuza hivyo kila mmoja na wote kwa jumla ili kuwafanya kwa
pamoja mashahidi wa Kristo hadi mipaka ya mwisho ya dunia. Tangazo la jina lake, la maisha yake, la msalaba wake mtukufu, la fumbo lake
na la mafundisho yake ndiyo huduma kuu wanayoweza kuwapatia ndugu zao
katika ubinadamu. Hilo linaendana na mipango ya kuendeleza watu na vitendo vidogovidogo vya
kila siku ambavyo wanawashirikisha waliyojaliwa na mikono ya Mungu kwa
njia ya kazi zao au kwa misaada ya watu wengine waliosogezwa jirani na
utandawazi. Ndugu Wadogo wa Afrika, wakijua kwamba wanachoweza kufanya ni kidogo kweli,
wanatia maanani ushirika na viungo vyote vya familia ya Mungu, yaani
Kanisa linaloongozwa na Papa na Maaskofu wenzake: ndani yake mchango wao
mdogo kwa ustawi wa utawala wa Mungu unaweza kuwafaidisha wengi, kwa
sababu upendo unazidishwa na uenezi wake. Upendo huo unatakiwa kupamba kama moto ili kufuta aina yoyote ya ubinafsi na
umimi inayowafunga watu ndani yao wenyewe na ya faida zao, ikiwafanya sio
tu wasiweze kuzaa lolote bali waharibu maisha yao na ya wenzao,
unavyothibitisha utamaduni wa Magharibi ambao umegeuka utamaduni wa kifo. Kinyume chake, wao wanataka kudumisha, kustawisha na kueneza tunu bora za makabila ya Afrika ili wachangie utamaduni wa uhai na wa mshikamano usio na mipaka. Ni
kwa Maria, mama wa Yesu, kwamba wanataka kujifunza unyenyekevu wapokee
neema ya moyo safi wenye kuwaka upendo ili kumshangilia Mungu na
kumtumikia kila mtoto wake.
|
||
The Little Brothers and Sisters of Africa are Franciscan missionaries of the Catholic Church based in Morogoro (Tanzania).
They form an association of life consecrated to God through the promise to observe the evangelical counsels of chastity, poverty and obedience according to a genuine enculturation of the charisma of fraternity and minority, which they have inherited from St. Francis of Assisi.
Their way of life aims at following Jesus through the fulfilment of his Gospel, all together and in solidarity with the most poor of the world today, so to become good news to them and to all people who hope for a world of justice, peace and love.
Believing that it will remain only a hopeless dream if men and women try to build it by themselves, the Little Brothers and Sisters of Africa pray day and night so that the assiduous contact and dialogue with the common Father may give to their minds the joy of his truth, unity of hearts, purity and strength in serving generously the most needy, and make them instruments of his peace.
It is the Holy Spirit, shared by Jesus dead and risen, who transforms anyone and everyone in such a way as to turn them into Christ’s witnesses up the last boundaries of the earth.
The proclamation of his name, his life, his glorious cross, his mystery and his teaching is the best service they can offer to their brothers and sisters in the world.
It is accompanied by works of human promotion and by little everyday deeds of sharing what they have received from God’s hand through their own work or contributions from people made nearby by the globalisation.
The Little Brothers and Sisters of Africa, knowing that what they can do is really something very little, value communion with all the members of God’s family, the Church guided by the Pope and his fellow Bishops: in unity with her, their little contribution for the building up of God’s kingdom can help many people by spreading love.
It is this love blazing like fire that eliminates any form of individualism and egotism which closes a person in himself and his profits, and so makes him not only sterile but also harmful to him and to others, as shown by today’s western culture, which has become a culture of death.
On the contrary, the Little Brothers and Sisters of Africa want to conserve, develop and diffuse the best values of the African peoples, in order to contribute to the establishment of a culture of life and solidarity at a global level.
It is from Jesus’ mother, Mary, that they want to learn humility, to be able to receive the gift of a pure heart burning with love, exulting in God and serving every child of God.
|
||
La loro è un’associazione di vita consacrata a Dio tramite la promessa di
osservare i consigli evangelici di castità, povertà ed obbedienza
secondo una sana inculturazione del carisma di fraternità e minorità
ereditato da san Francesco di Assisi. La loro forma di vita si propone di seguire Gesù con la pratica comunitaria del suo Vangelo in solidarietà coi più poveri di oggi così da essere una buona notizia per essi e per tutti quelli che anelano ad un mondo di giustizia, pace ed amore. Credendo che esso resterà solo un sogno se gli uomini e le donne
cercheranno di costruirselo con le proprie forze, i Piccoli Fratelli e
Sorelle d’Africa ricorrono alla preghiera giorno e notte perché l’assiduo
contatto e colloquio col Padre comune doni alle menti la gioia della
verità, unisca i cuori, purifichi e rafforzi in tutti l’intenzione di
servire generosamente i più bisognosi, e ne faccia strumenti della sua
pace. E’ lo Spirito Santo, comunicato tramite Gesù morto e risorto, a compiere
tale trasformazione di ognuno e di tutti per renderli insieme testimoni di
Cristo fino agli estremi confini della terra. L’annunzio del suo nome, della sua vita, della sua croce gloriosa, del suo
mistero e del suo insegnamento costituisce il massimo servizio che possono
rendere ai loro fratelli e sorelle in umanità. Ad esso si affiancano opere di promozione umana e piccoli gesti quotidiani
di condivisione di quanto ricevuto dalla mano di Dio attraverso il proprio
lavoro o i contributi di gente resa vicina dalla globalizzazione. I Piccoli Fratelli e Sorelle d’Africa, coscienti che quanto possono fare
è veramente poco, valorizzano la comunione con tutti i membri della
famiglia di Dio, la Chiesa guidata dal Papa e dai suoi colleghi Vescovi:
in essa il loro piccolo contributo alla crescita del Regno di Dio può
riuscire di vantaggio a tanti, perché l’amore diffondendosi si
moltiplica. E’ un amore che deve divampare come il fuoco per eliminare ogni forma di
individualismo e di egoismo che chiude in sé stessi e nei propri
interessi, rendendo non solo sterili ma dannosi a sé e agli altri, come
dimostra la cultura occidentale divenuta una cultura di morte. Al contrario, essi vogliono conservare, sviluppare e diffondere i migliori
valori dei popoli africani per contribuire ad una cultura della vita e
della solidarietà globale. E’ da Maria, la madre di Gesù, che vogliono imparare l’umiltà per
accogliere il dono di un cuore puro ed ardente di amore per esultare in
Dio e servire ogni suo figlio.
|
||
Los Pequeños Hermanos y Hermanas de África son misioneros franciscanos de la Iglesia Católica con sede en Morogoro (Tanzania).
|
||