Ndugu Wadogo Wa Afrika

Historia kwa ufupi (ya jana na ya kesho)

 

Ndugu Wadogo wa Afrika walianza kukusanyika tarehe 4-10-1991 kwenye kijiji cha Izazi (mkoa wa Iringa, nchini Tanzania), halafu wakahamia Mkungugu (mkoa huohuo) na kuanzia tarehe 31-10-1995 katika mtaa mmojawapo wa mji wa Morogoro. 
Muda wa jaribio ulimalizika tarehe 9-7-1997, askofu Telesphor Mkude wa Morogoro alipounda rasmi chama chao pamoja na kuthibitisha katiba yake. 
Wakati wa adhimisho la ekaristi waanzilishi 11 (6 wa kike na 5 wa kiume) waliweka ahadi ya kuishi kijumuia Injili kadiri ya Kanuni ya Utawa Hasa wa Tatu wa mtakatifu Fransisko, iliyothibitishwa na papa Yohane Paulo II, na kadiri ya katiba hiyo maalumu. 
Baada ya nyumba asili mbili, ziliongezeka ile ya kiume ya Kiroka (27-1-1998), ile ya kike ya kijiji hichohicho (15-9-1998) na ile ya kiume ya Langali (10-7-2000), zote zikiwa katika mkoa wa Morogoro. 
Tangu tarehe 4-11-2004 wameanza kuwepo hata Kapelekesi katika jimbo la Mbeya, mipakani kwa Malawi. 
Mnamo tarehe 15 Januari 2009 waliowekwa wakfu kwa ahadi ya daima walikuwa 14 (6 wa kiume na 8 wa kike), wanachama wenye ahadi ya muda walikuwa 22 (7 kwa 15), na ndugu kwenye jaribio 10 (1 kwa 9). 
Hamu kuu ya ndugu hao ni kumshuhudia Yesu kwa maneno na kwa maisha yao yote, katika Afrika nzima na mpaka miisho ya dunia, kwa kuwa kila mtu anamhitaji yeye, mwokozi wa ulimwengu, na kwa hiyo ana haki ya kumjua ili awe kitu kimoja naye na Baba aliyemtuma. 
Kwa ajili hiyo wanatarajia kupata mapema Wafransisko wa ulimwenguni, hasa wenye ndoa, ambao washuhudie tunu zilezile za kwao katika maisha ya kila siku ya watu wa kawaida: katika familia, uchumi, siasa n.k.

Ndugu Wadogo wa Afrika wamejiunga na Baraza la Kifransisko la Kimataifa la Utawa Hasa wa Tatu (International Franciscan Conference of the Brothers and Sisters of the Third Order Regular).   

LINKS:

 

WIMBO WA TAIFA

Mungu Ibariki Afrika

Wabariki viongozi wake

Hekima, umoja na amani

Hizi ni ngao zetu

Afrika na watu wake. 

CHORUS:    

Ibariki, Afrika

Ibariki, Afrika

Tubariki, watoto wa Afrika

Izazi: La prima Cappella - Izazi: Kikanisa cha kwanza - Izazi: The first chapel