Ndugu Wadogo Wa Afrika

Maisha na utendaji

 

Wakiwa viumbe na watoto wa Mungu, wanaofurahi kumtegemea kabisa, ndugu wadogo wanatafuta katika sala uso wake na matakwa yake, pamoja na nguvu ya kuyatekeleza.

 

Ratiba ya jumuia ina walau dakika 250 za sala, zilizogawanyika kati ya usiku na mchana ili ziongoze mwendo wa maisha ya kila siku, zikimuachia kila mmoja nafasi nyingine za kuongea na Baba kwa njia ya Mwana katika Roho Mtakatifu.

 

Maisha ya Kiroho yanazaa ushirika wa kidugu na utendaji wa nje: nyakati za kusoma, kufanya kazi na kuburudika kwa uwiano wa kufaa.

 

Masomo yanahusu kwanza kabisa Neno la Mungu, ambalo ndio msingi wa malezi ya awali na ya kudumu, na ambalo linaangaza mambo yote na namna ya kuyakabili kwa hekima.

 

Kazi zinajumlisha zile za mikono kwa ajili ya mahitaji ya jumuia na ya fukara, zile kwa ajili ya ustawi wa jamii (ushauri nasaha kwa familia, kituo cha kulelea watoto wadogo, shule ya kompyuta, sekondari isiyotoza ada yoyote), na hasa zile za uinjilishaji (katika parokia, jumuia ndogondogo za Kikristo, madarasa, redio, wiki za uamsho kwa vijiji vya mbali).

 

Sikukuu na burudani za kijumuia (mbili kwa siku) ndiyo nafasi ya kuacha furaha ya kuwa ndugu ilipuke na ya kuchanga kwa upendo imani na maisha.

  Majukumu ya kila siku

  • MALEZI. Safari ya kila mmoja kuelekea ukomavu, kwa kuongozana na waliomtangulia na jamaa nzima, inayohitajika ili upendo usibaki neno tupu, bali ufikie ukamilifu.  

  • SALA. Fungamano na Mungu, lililo hamu ya dhati zaidi moyoni mwa binadamu, la kustawishwa kwa makusudi na uangalifu na mtu mmoja mmoja na jumuia pia, ili lizae matunda ya uzima wa milele.  

  • KAZI. Tunu ya kudumishwa katika ulimwengu wa starehe, juhudi kwa utekelezaji wa chochote kinachohitajika au kinachomfaa mtu, inazidi kuwa na maana ikipangwa na kufanywa kwa pamoja, kadiri ya matakwa ya Baba.

LINKS:

 

WIMBO WA TAIFA

Mungu Ibariki Afrika

Wabariki viongozi wake

Hekima, umoja na amani

Hizi ni ngao zetu

Afrika na watu wake. 

CHORUS:    

Ibariki, Afrika

Ibariki, Afrika

Tubariki, watoto wa Afrika

Morogoro, 10 luglio 1997: gli undici fondatori con un prete anziano nella casa del vescovo per le prime elezioni della neonata associazione. - Morogoro, 10 Julai 1997: waanzilishi 11 pamoja na padri mzee katika nyumba ya askofu kwa ajili ya uchaguzi wa kwanza wa chama kichanga. - Morogoro, July 10th: the 11 founders with an old priest in the house of the Bishop for the first elections of the new association.