MASWALI
JUU YA MASHAURI YA KIINJILI
|
1. USEJA MTAKATIFU
1.1.
USEJA KWA AJILI YA UFALME WA MBINGUNI NI WITO WA KUWAPENDA:
1.1.1. YESU NA
MARIA
1.1.1.1. Una
uhusiano gani na Kristo?
1.1.1.2.
Unaudhihirisha vipi katika maisha ya kila siku?
1.1.1.3.
Unafanya nini ili uhusiano huo uzidi kustawi?
1.1.1.4. Je,
unachochea mfululizo imani, tumaini na upendo ndani yako?
1.1.1.5. Je,
unapigania uhuru wa ndani kuhusu mivuto ya watu na vitu ili ujenge uhusiano wa
dhati zaidi na Yesu?
1.1.1.6. Je,
unampenda Yesu ndani ya watu na kuwapenda watu ndani yake?
1.1.1.7.
Uhusiano wako na bikira Maria unakusaidia vipi kuutunza safi moyo wako na mwili
wako?
1.1.2.
WANAJUMUIA WENZAKO
1.1.2.1. Una
uhusiano gani na watu wa jumuia yako?
1.1.2.2. Je,
kati yenu kuna upendo halisi wa kidugu?
1.1.2.3. Upendo
huo unadhihirika kwa matendo gani?
1.1.2.4.
Jumuiani mnasaidiana vipi ili kufanikisha maisha ya kitawa kwa kukuza upendo kwa
Mungu na kwa
jirani?
1.1.2.5. Je,
katika jumuia yako wapo wanaojisikia wapweke? Kwa nini?
1.1.2.6.
Unawafanyia nini?
1.1.2.7.
Unawaonaje walio wagonjwa au wakongwe katika jumuia yako?
1.1.2.8.
Unaonaje urafiki katika jumuia na nje ya jumuia yako?
1.1.2.9.
Masharti gani yatafanya urafiki uwe na faida kwa mtu binafsi na kwa jumuia?
1.1.3. WATU
WOTE
1.1.3.1. Je, u
wazi kweli kwa wote mahali unapoishi na unapofanya kazi?
1.1.3.2. Je,
una moyo wa kujitolea uhudumie kwa bidii wale wote wanaokuhitaji hata
wasipoonyesha
shukrani?
1.1.3.3. Je,
unatoa uangalifu, wema na msaada sawasawa kwa wote, bila ya kujali ni wa kabila
gani?
1.1.3.4.
Unawajibika vipi kwa ajili ya jamaa zako?
1.1.3.5.
Unajisikia kuzuiwa na masharti ya useja katika kuwapenda? Kwa nini?
1.2.
USEJA KAMA USHUHUDA
1.2.1.
Watu wa kwenu wanauonaje useja kwa ajili ya ufalme wa mbinguni, na hali
yako ya useja?
1.2.2.
Useja una maana gani kwao?
1.2.3.
Ikiwa wanaona vigumu kuukubali au kuuelewa, ni kwa sababu gani?
1.2.4.
Je, ni kwa sababu za jadi au za dini?
1.2.5.
Au pengine ni kwa sababu watawa hawatoi ushuhuda ulio wazi wa kutosha?
1.2.6.
Je, unatimiza wajibu wa kuwa na utaratibu wa nje pamoja na msimamo mzuri
mpaka ndani ya moyo?
1.3.
USEJA KATIKA MAISHA YAKO BINAFSI
1.3.1.
Je, umeridhika na malezi uliyoyapata utawani kuhusu maswala yote
yanayohusu jinsia?
1.3.2.
Mawazo yako kuhusu jinsia yana utulivu au fujofujo na hofu zaidi?
1.3.3.
Je, unaweza kuwashauri vijana na watu wa ndoa kuhusu usafi wa moyo?
1.3.4.
Ujuzi wako kuhusu useja umebadilika vipi tangu uingie utawani?
1.3.5.
Unaelewaje useja kwa sasa?
1.3.6.
Je, unajisikia umekomaa vya kutosha ukabili maisha ya useja?
1.3.7.
Je, useja mtakatifu unatosha kutimiza haja yako ya kupendwa na kupenda?
1.3.8.
Je, unafahamu na kupokea tunu na maadili ya jinsia yako halafu uko tayari
kuyatimiza kitawa?
1.3.9.
Sababu gani hasa zimekufanya uamue kuishi kwa useja?
1.3.10.
Je, namna yako ya kuongea, kuhusiana na watu, kuwaonyesha upendo,
inalingana na nia hiyo?
1.3.11.
Je, umetambua useja wako unavyokusaidia wewe na watu unaokutana nao
kukomaa kiutu na kufikia ufalme wa Mungu?
1.3.12.
Ukiweza kutimiza useja kitakatifu, unamshukuruje Mungu kwa karama hiyo?
1.3.13.
Unafanya juhudi gani ili kuipokea kwa uaminifu isiharibike?
1.3.14.
Je, useja unakusaidia kuzingatia kwa moyo mkuu matakwa yote ya Bwana?
1.3.15.
Je, unatumia vizuri muda ulioachiwa ujipangie?
1.3.16.
Unaamini maneno ya Bwana kuhusu useja na kutegemea msaada wake au
unajiamini kwa kuwa, eti, umeshazoea?
1.3.17.
Je, unashikwa mno na watu, matukio na vitu?
1.3.18.
Je, umetambua kwamba useja mtakatifu hauwezekani pasipo kujikana?
1.3.19.
Katika mazingira yako mambo gani yanakuzuia zaidi usikue katika upendo
inavyodaiwa na useja?
1.3.20.
Unapambana nayo vipi?
1.3.21.
Je, katika ulimwengu huu wa anasa, unafukuza mara yale yote yanayoweza
kuhatarisha usafi wa moyo wako?
1.3.22.
Je, unatumia uangalifu na busara kuhusu
vyombo vya upashanaji habari?
2.
UFUKARA
2.1
UFUKARA NA WATU
2.1.1.
Katika eneo lako watu gani ni fukara kweli?
2.1.2.
Kitu gani kinawafanya wawe hivyo?
2.1.3.
Je, wanakuhesabu ni mmojawao? Kwa nini ndiyo au siyo?
2.1.4.
Je, unajisikia kuwapenda kwa dhati?
2.1.5.
Unapendelea kuwa nao au kuwa na watu wa juu?
2.1.6.
Unajifunza nini kwao?
2.1.7.
Unawakumbuka mara ngapi wale wote wanaokosa hata mahitaji makuu?
2.1.8.
Je, uko tayari kuwaachia vyote ulivyo navyo?
2.1.9.
Unadhani jumuia yako inatakiwa kusaidia ndugu zako wenye shida? Vipi?
2.1.10.
Au unawakumbuka wale wa ukoo wako tu?
2.1.11.
Fukara akikuomba msaada, kwa kawaida unafanya nini?
2.1.12.
Unafikiri ni wajibu wako kama mtawa kuupiga vita ufukara? Kama ni hivyo,
unaweza kufanya nini?
2.1.13.
Kwa sasa unafanya nini? Mnafanya nini kijumuia?
2.1.14.
Unadhani mnafanya vya kutosha au mnapaswa kufanya zaidi? Mnaweza kufanya
nini?
2.1.15.
Je, unajitahidi kuchochea dhamiri za watoto na watu wazima waitikie mlio
wa umati wa fukara?
2.1.16.
Unajisikiaje katika ulimwengu wa leo unaotawaliwa na mali na pesa?
2.1.17.
Unakubali kwamba Kanisa linapaswa kuendeleza kazi ya Kristo katika
ufukara na dhuluma?
2.1.18.
Nyinyi kama watawa mnaweza kufanya nini ili ushuhuda wenu wa ufukara uwe
na maana zaidi?
2.2.
UFUKARA KWAKO MWENYEWE
2.2.1.
Ufukara wa kitawa una maana gani kwako?
2.2.2.
Ujuzi wako kuhusu ufukara umebadilika vipi tangu uingie utawani?
2.2.3.
Sababu gani hasa zimekufanya uamue kuishi kwa ufukara?
2.2.4.
Ufukara unakusaidia vipi katika uhusiano wako na Mungu na jumuia ya
kitawa na watu wa nje?
2.2.5.
Usipokusaidia ni kwa sababu gani?
2.2.6.
Je, kwa kushika ufukara wa hiari unajisikia mwepesi na huru moyoni?
2.2.7.
Je, uliwahi kuonja heri ya ufukara?
2.2.8.
Ukikumbuka ahadi ya Yesu kwamba utapata mara mia zaidi, unatarajia nini?
2.2.9.
Unakumbuka mara ngapi kwamba umejiwekea hazina mbinguni?
2.2.10.
Unafuata njia gani za kukua katika
umaskini wa roho?
2.2.11.
Unafurahi kumtegemea Mungu tu, au unajiulizauliza kuhusu uchumi wa
shirika lako siku za mbele?
2.2.12.
Unaweza kuufafanua vipi ufukara wako kwa
familia yako au kwa maskini hata wakuelewe?
2.2.13.
Ulipowahi kujaribu kuwaeleza, walisema
nini?
2.2.14.
Je, wanatambua kwamba huna tamaa?
2.3.
MADAI YA UFUKARA WA KITAWA
2.3.1.
Je, unafanya kazi kwa bidii kama Yesu huko Nazareti, ukishikamana na
wazazi wengi fukara?
2.3.2.
Katika kazi unalenga nini kuliko faida ya uchumi?
2.3.3.
Je, kisha kufanya kazi, unajiona ni haki yako kudai vitu kadiri ya mapato?
2.3.4.
Kabla hujaomba kitu, unafikiria kama ni mapenzi ya Mungu ukiombe, au
unabuni tu njia ya kupewa?
2.3.5.
Je, unapokea vyote kwa shukrani bila ya kudai zaidi?
2.3.6.
Je, unatambua thamani ya vitu na manufaa yake kwa wote?
2.3.7.
Je, unavitumia kwa utaratibu visiharibike kabla ya wakati?
2.3.8.
Je, unaridhika na vitu vya lazima tu kadiri unavyopewa?
2.3.9.
Au unakosa raha usipopata vingine unavyoviona muhimu kwako?
2.3.10.
Ukipewa vitu vizuri, unafanya nini ili
kushinda mvuto wake?
2.3.11.
Je, ukiweza kuchagua mwenyewe, unapendelea vitu vilivyo sahili zaidi?
2.3.12.
Je, ukipewa vingi kuliko unavyovihitaji,
uko tayari kuvirudisha jumuiani?
2.3.13.
Je, wakikupa zawadi yoyote, unaikabidhi
jumuiani?
2.3.14.
Je, ukikabidhiwa pesa, unajitahidi
kuitumia kwa uangalifu na kutoa ripoti sahihi?
2.3.15.
Je, unashikilia vitu au mbinu
fulanifulani hata ukavitegemea mno?
2.3.16.
Je, unajitahidi kujikana na kujibandua na
wote na vyote ili uungane zaidi na Yesu?
2.3.17.
Je, unatamani elimu na mamlaka ili uwe
juu ya wengine?
2.3.18.
Je, uko tayari kujinyima nafasi na
mafanikio ili ujitolee kwa wengine?
2.3.19.
Kwa sasa unashirikishana nini na watawa
wenzako?
2.3.20.
Mnaweza kushirikishana nini zaidi ili
kuimarisha umoja wa jumuia?
2.3.21.
Jumuia yako inaweza kufanya nini ili
ufukara wenu uwe wa Kiinjili zaidi?
2.3.22.
Ufukara wa kitawa unakudai nini zaidi?
3. UTIIFU
3.1.
MAANA YA UTIIFU
3.1.1.
Utiifu una maana gani kwako?
3.1.2.
Unakudai unyenyekevu wa aina gani?
3.1.3.
Kuna tofauti gani kati ya utiifu wa kitawa na ule wa mwanafunzi, wa
mfanyakazi au wa mwanajeshi?
3.1.4.
Kwa namna gani kiongozi wa kitawa ni mwakilishi wa Mungu kwako?
3.1.5.
Unaweza kumchora vipi mtawa mtiifu kweli?
3.1.6.
Unafikiri maelezo yako yanalingana na mafundisho ya Agano Jipya?
3.1.7.
Utiifu wa kitawa unakusaidia vipi kujitoa zaidi kwa Mungu, kwa Kanisa na
kwa jirani?
3.1.8.
Unaonaje uhusiano wa utiifu na umisionari?
3.2. UTIIFU NA
MATAKWA YA MUNGU
3.2.1.
Unazingatia vipi mifano ya Yesu na Maria katika kuambatana kwa moyo na
matakwa ya Mungu?
3.2.2.
Matakwa ya Mungu yanaunganisha vipi maisha yako yote usije ukasambaratika?
3.2.3.
Utawani matakwa ya Mungu yanadhihirika kwako kwa njia zipi? Ipi ni ya
kawaida na ya hakika zaidi?
3.2.4.
Unatumia muda gani kumsikiliza Mungu akisema nawe kupitia njia hizo?
3.2.5.
Unafanya hivyo kwa namna gani?
3.2.6.
Je, unatambua jinsi utiifu unavyokusaidia kuungana na Mungu na kumpendeza
kama Mwana wake?
3.2.7.
Unapotii unafuata nidhamu tu au unamtolea Baba sadaka ya hiari yako kwa
moyo wa kitoto?
3.2.8.
Je, unapenda kuangazwa na kuongozwa na sheria za utawa katika maisha yako?
3.2.9.
Je, uko tayari kushirikiana na wenzako na kuwasaidia wenye shida, kuanzia
wale wa jumuia yako?
3.2.10.
Je, uko tayari kupokea watu na matukio
kadiri Mungu alivyopanga?
3.2.11.
Je, uko tayari kubadili mipango yako ili ukabili hali na mambo
usiyotarajia?
3.2.12.
Je, uko tayari kubadili mipango yako ili
utekeleze ile ya jumuia na ya kiongozi?
3.2.13.
Ikiwa unaelekea kushikilia mipango yako
tu, ni kwa sababu gani?
3.2.14.
Unaona njia gani ya kutimiza ahadi ya
kumtii Papa?
3.3.
UTIIFU NA UONGOZI
3.3.1.
Je, unajitahidi kuwa tayari kuwatii viongozi hata kabla hawajakuagiza?
3.3.2.
Je, unaona ni rahisi kutii katika jumuia yako na jamaa yako? Kwa nini
ndiyo au siyo?
3.3.3.
Je, uko wazi kwa viongozi wako au unawakwepa, unawadanganya na kuwasema?
3.3.4.
Je, una wepesi wa kuelewa na kukubali maamuzi yao?
3.3.5.
Ukishindwa kufanya hivyo, je, unajua kujieleza kwa unyenyekevu na upendo?
3.3.6.
Kwa sababu gani unaweza ukabishana nao au hata kupinga sheria za utawa?
3.3.7.
Unaweza na unatakiwa kufanya nini kuhusu tatizo hilo?
3.3.8.
Je, unajitahidi kuonja na kurudisha upendo wa Baba katika viongozi wako?
3.3.9.
Utiifu unakusaidia vipi kutimiza karama yako kama mtawa?
3.3.10.
Kadiri ya Injili, utiifu unadai kujikana:
neno hilo linatimia vipi katika maisha yako?
3.3.11.
Je, uliwahi kutii kwa moyo wote amri isiyokupendeza? Ulijisikiaje?
Matokeo yake nini?
3.3.12.
Je, unaamini kwamba kutii kwa mateso ni
njia ya kukomaa kiutu na Kiroho?
3.3.13.
Je, unaamini kwamba kutii kwa mateso ni
njia ya kukomboa ulimwengu pamoja na Kristo?
3.3.14.
Je, msimamo wako kwa viongozi wa jumuia,
jamaa na Kanisa unalingana na Injili?
3.3.15.
Kitu gani kinakufanya uwe na msimamo huo:
upendo, imani na unyenyekevu halisi au tabia ya kukwepa matatizo, kutojali na
kiburi?
3.4.
UTIIFU NA UHURU
3.4.1.
Utiifu unakusudiwa kujenga uhuru wa ndani: je, unajisikia huru kutii? Kwa
nini ndiyo au siyo?
3.4.2.
Unauelewaje uhuru katika maisha ya kitawa? Uelewa wako unafuata imani au
hoja za kibinadamu?
3.4.3.
Je, unafikiri utiifu wa kitawa unalinda uhuru wako? Vipi?
3.4.4.
Ukitumia uhuru wako kwa kusisitiza umuhimu wa mambo yako binafsi, kuna
sababu gani?
3.4.5.
Je, unajisikia umepewa madaraka ya kutosha katika kazi zako? Kwa nini
ndiyo au siyo?
3.4.6.
Je, unachukua kwa urahisi majukumu kuhusu kazi zako na maisha ya jumuia
yako au unapendelea kuwaachia wengine kuamua na kukuambia la kufanya? Kwa nini?
3.4.7.
Je, unajua kutofautisha mbele ya Mungu lini utekeleze maagizo
yalivyotolewa, na lini uchukue jukumu la kufanya tofauti kidogo kutokana na hali
ilivyo?
3.4.8.
Je, unajua kuwajibika bila ya kupuuzia matakwa ya viongozi wako wala
kuwachukiza?
3.4.9.
Je, unajua kuchangia utambuzi wa matakwa ya Mungu kwa kujadiliana vema na
viongozi na jumuia?
3.4.10.
Je, ungependa maamuzi yote jumuiani
yachukuliwe kidemokrasi?