Chama, kilichoanza wakati wa
upapa wa Yohane Paulo II, kinafuata Kanuni aliyowathibitishia ndugu wa
kiume na wa kike wa Utawa Hasa wa Tatu wa mtakatifu Fransisko.
Zaidi ya hayo, kimechota kwa
wingi katika maisha yake ya Kiroho yaliyozama ndani ya fumbo la Kristo na
Maria na kujitokeza katika ngao yake ya kipapa yenye herufi M (yaani Maria)
chini ya msalaba.
Kwa hiyo wanachama wanavaa saa
zote kanzu ya Kifransisko ambayo upande wa moyo ina lebo inayotumia ishara
hizohizo juu ya ramani nyeusi ya Afrika.
Bara hilo, ambalo pengine lina
hali ngumu kiasi cha kutisha, linatawaliwa tayari tena italibidi lizidi
kutawaliwa na msalaba wa Kristo, mwekundu kwa damu na kama moto wa Upendo
wa Mungu unaotakiwa kupamba duniani kote.
Chini yake, M nyeupe
linamaanisha moyo safi wa Maria, uliomwezesha kutazama kwa dhati na
kushiriki kikamilifu mpango wa Mungu ulipotimia katika sadaka ya utiifu wa
Mwanae kwa wokovu wa binadamu wote.
Lebo ni mwaliko na hamu ya kuwa
wana halisi wa Maria, wenye moyo safi wa kimama kama wa kwake mbele ya
msalaba wowote ambao Yesu anaendelea kuteseka ndani ya wale aliowaita
ndugu zake wadogo, akitangaza kwamba mwishoni tutahukumiwa kuhusu yale
yote ambayo tumemtendea au kuacha kumtendea kila mmojawao.
|