Uongozi wa shule
Shule yetu ni mali ya Jimbo Katoliki la Morogoro (S.L.P. 640 –
Morogoro; www.morogoro.tk ). Siku za mbele inaweza ikaachwa moja kwa
moja mikononi mwa Alfagems Co. Ltd., kampuni lililosajiliwa likiwa
na makao makuu katika manispaa ya Morogoro, mtaa wa Kilakala,
barabara ya Kilakala (S.L.P. 6083 - Morogoro).
Tangu sasa shule inaendeshwa na mmoja kati ya Wakurugenzi wa kampuni
hilo (ambalo ni mali ya Jimbo kwa asilimia 80), akishirikiana na
Mkuu wa Shule na walimu wengine pamoja na wawakilishi wa familia za
wanafunzi kupitia Bodi ya Shule.
Shule inatarajiwa kuendelea kupata walimu wa kutosha wenye digrii au
diploma, maadili, vipawa na juhudi za kuridhisha.
Hali ya kifamilia katika mafungamano, mvuto wa malengo maalumu ya
kituo, na hakika ya malipo kwa wakati wake ni kati ya sababu
zitakazowafanya walimu wapende kujiunga na shule.