Mitaala
Asubuhi shule yetu inafuata mitaala iliyotolewa na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kidato cha kwanza hadi kidato cha
sita), kwa kuzingatia imani na maadili ya Kanisa Katoliki, pamoja na
mila njema za Watanzania ili nchi iweze kujengwa kwa uimara.
Masomo ya Bible Knowledge na Divinity ni ya lazima kwa Wakristo
wote.
Aidha, masomo ya Dini yanafundishwa kadiri ya imani ya wanafunzi na
utayari wa walimu wa kujitolea kutoka dini husika
Lugha ya Kiingereza ndiyo itakayotumika kufundishia kwa kuzingatia
maelekezo ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Shule yetu ni ya sekondari kuanzia kidato cha 1 hadi cha 6. Kuanzia
mwaka 2010 asubuhi kutakuwa na mikondo 24 (6x4) .
Shule yetu inapokea hata watu waliochelewa kupata elimu (wanandoa,
wafanyakazi n.k.), madarasa yanatumika hata jinni na Jumamosi kwa
kozi za haraka kuliko kawaida.
Kwa hiyo, mikondo inaweza kuwa 48, na wanafunzi wote 2160.Kwa sasa
wasichana 400 wanaishi katika mabweni ya shule, wengine na wavulana
wote wanatokea nyumbani.