Malengo ya shule
Nia ya kuanzisha shule yetu ni kuwapatia malezi na elimu ya
sekondari hasa wasichana wanaoshindwa kuvipata sehemu nyingine
kutokana na hali ngumu ya uchumi.
Kwa ajili hiyo, elimu inatarajiwa kutolewa kwa kudai tu karo
iliyopangwa na serikali kwa ajili ya shule za binafsi, si zaidi. Kwa
sasa ni 1/3 hadi 1/5 ya ada za shule nyingine za binafsi.
Shule yetu si kwa ajili ya watoto wa vigogo, bali ya matabaka ya
chini, ili kuwapa watu wengi iwezekanavyo fursa ya kupata maendeleo
na kuchangia ujenzi wa jamii yetu.
Shule yetu haiwabagui walengwa kwa msingi wa dini, wa kabila n.k.
Kati ya wanafunzi wapo watawa wa Kanisa Katoliki ili kuinua nidhamu
na maadili, ambavyo vinazingatiwa sana.
Baadhi ya wanafunzi watakaofaa zaidi wataweza kuendelezwa na
hatimaye kuajiriwa na kampuni kadiri litakavyohitaji.