Nafasi za Masomo
JIMBO KATOLIKI LA MOROGORO
ALFAGEMS SECONDARY SCHOOL (S.3874)
S.L.P. 6083 – MOROGORO
Tel. 0732-931605 (Ofisi) / 0789-978886 (Airtel Money)
0655-425723 (kuwasiliana Tigo Pesa) / 33708 (uwakala wetu Tigo Pesa)
0752-452444 (kuwasiliana M-Pesa) / 237405 (uwakala wetu M-Pesa)
0714-176745 (Bweni la kiume la chini) / 0786-906311 (Bweni la kiume
la juu)
Ø
Shule yetu inazingatia taaluma na maadili kwa kufuata sera ya elimu
ya Kanisa Katoliki.
Ø
Tunawashukuru nyinyi, wananchi wote, kwa kuonyesha mmeipenda sana.
Ø
Tunasikitika kulazimika kupandisha ada kutokana na ongezeko la
mishahara na mfumuko wa bei.
Ø
Sababu nyingine ni kwamba tangu mwaka 2009 tunazidi kuomba ruzuku ya
serikali lakini bado.
Ø
Kumbe tumeongezewa kodi (SDL) isiyozingatia mapato bali matumizi (5%
ya mishahara yote): hivyo pesa zote za fomu zitapelekwa serikalini
kulipia kodi hiyo.
Ø
Pamoja na kuwaahidia juhudi endelevu za kuboresha huduma,
tunawatangazia nafasi zifuatazo.
Ø
Tafadhali, kabla hamjanunua fomu, ulizeni vizuri kuhusu masomo
yanayowafaa zaidi.
Ø
Baadaye hamtaruhusiwa kubadili fomu wala masomo, kwa sababu ni
lazima twende kwa mpango.
MASOMO YA SEKONDARI KUANZIA ASUBUHI
Ni elimu rasmi kwa wale tu wenye sifa za kufanya mitihani ya taifa
kama wanafunzi wa shule; wengine wafikirie masomo ya jioni.
F I:
KUINGIA KIDATO CHA
F V:
KUINGIA KIDATO CHA TANO (History, Kiswahili na Language; au
History, Geography na Kiswahili; au History, Geography na Language;
au History, Geography na Economics; au Economics, Geography na
Mathematics; au Chemistry, Biology na Geography; au Physics,
Chemistry na Biology; au Physics, Chemistry na Mathematics).
Wanaotaka kujiunga wawe: wamezaliwa si kabla ya mwaka 1993;
wamefaulu (A, B+, B, C au D) English na masomo yale yote
waliyoyachagua; wamepata credits (A, B+, B au C) walau mbili katika
masomo waliyoyachagua na ya tatu katika somo lolote walipofanya au
waliporisiti mtihani wa kidato cha nne; wamepata credit ya tatu
mwaka 2013 au 2014. Usaili utafanyika tarehe 13-6-2015 saa 2:00
asubuhi na utategemea vyeti (vya kuzaliwa, vya kuacha shule na hati
za matokeo ya kidato cha nne). Washindi wataanza masomo tarehe
30-6-2015.
TUISHENI WAKATI WA LIKIZO
(Civics, History, Geography, English, Kiswahili, Biology, Chemistry,
Physics, Mathematics na Information & Computer Studies). Mpango huo
mpya utaanza tarehe 1-12-2014 kwa wanafunzi wa shule yoyote ili
kuwainua kitaaluma wakiwa likizo.
MASOMO YA SEKONDARI KUANZIA ALASIRI
(JUMAMOSI KUANZIA ASUBUHI)
Ni kwa wale watakaofanya mtihani wa maarifa (maarufu kama Q.T.) na
mitihani mingine ya taifa kama watahiniwa wa kujitegemea. Bweni la
wavulana halina nafasi kwa ajili yao.
P I:
KUJIANDAA MIAKA MIWILI KWA MTIHANI WA MAARIFA (Civics,
History, Geography, English, Kiswahili, Biology na Mathematics).
Masomo yataanza tarehe 13-1-2015. Ada ni Tsh. 240,000 kwa mwaka.
Kwa kukaa bweni wasichana wataongeza Tsh. 500,000. Jumla ni Tsh
740,000.
I-II:
KUJIANDAA MWAKA MMOJA KWA MTIHANI WA MAARIFA (Civics,
History, Geography, English na Kiswahili). Masomo yataanza tarehe
13-1-2015. Ada ni Tsh. 240,000 kwa mwaka. Kwa kukaa bweni wasichana
wataongeza Tsh. 500,000, jumla ni Tsh 740,000.
P II:
KUJIANDAA MWAKA MMOJA TENA KWA MTIHANI WA MAARIFA (Civics,
History, Geography, English, Kiswahili, Biology na Mathematics).
Wanaotaka kujiunga wawe na elimu inayolingana walau na ile ya
kidato cha kwanza. Masomo yataanza tarehe 13-1-2015. Ada ni Tsh.
240,000 kwa mwaka. Kwa kukaa bweni wasichana wataongeza Tsh.
500,000. Jumla ni Tsh 740,000.
P III:
KUJIANDAA MIAKA MIWILI TENA KWA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE
(Civics, History, Geography, English, Literature, Kiswahili, Biology
na Mathematics; au Civics, History, Geography, English, Literature,
Kiswahili na Information & Computer Studies). Wanaotaka kujiunga
wawe na elimu inayolingana walau na ile ya kidato cha pili. Masomo
yataanza tarehe 13-1-2015. Ada ni Tsh. 240,000 kwa mwaka. Kwa kukaa
bweni wasichana wataongeza Tsh. 500,000. Jumla ni Tsh 740,000.
III-IV:
KUJIANDAA MWAKA MMOJA KWA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE
(Civics, History, Geography, English na Kiswahili). Wanaotaka
kujiunga wawe wamefaulu mtihani wa maarifa. Masomo yataanza tarehe
13-1-2015. Ada ni Tsh. 240,000 kwa mwaka. Kwa kukaa bweni wasichana
wataongeza Tsh. 500,000. Jumla ni Tsh 740,000.
P IV:
KUJIANDAA MWAKA MMOJA TENA KWA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE
(Civics, History, Geography, English, Kiswahili, Biology na
Mathematics; au Civics, History, Geography, English, Literature,
Kiswahili na Information & Computer Studies).
Wanaotaka kujiunga wawe na elimu inayolingana walau na ile ya
kidato cha tatu na wawe wamefaulu mtihani wa maarifa. Si watu wa
kurisiti ule wa kidato cha nne. Masomo yataanza tarehe 13-1-2015.
Ada ni Tsh. 240,000 kwa mwaka. Kwa kukaa bweni wasichana wataongeza
Tsh. 500,000. Jumla ni Tsh 740,000.
T (= TARATIBU): KUJIANDAA
MIAKA MIWILI KURISITI MTIHANI WA KIDATO CHA NNE
(Civics, History, Geography, English, Kiswahili, Biology na
Mathematics; au Civics, History, Geography, English na Kiswahili).
Wanaotaka kujiunga wawe wameshafanya ule wa kidato cha nne. Masomo
yataanza tarehe 13-1-2015. Ada ni Tsh. 240,000 kwa mwaka. Kwa kukaa
bweni wasichana wataongeza Tsh. 500,000. Jumla ni Tsh 740,000.
H (= HARAKA):
KUJIANDAA MWAKA MMOJA KURISITI MTIHANI WA KIDATO CHA NNE
(Civics, History, Geography, English na Kiswahili) wawe wamepata
credit (A, B+, B au C) walau moja katika somo lolote walipofanya au
kurisiti mtihani wa kidato cha nne. Masomo yataanza tarehe
13-1-2015. Ada ni Tsh. 240,000 kwa mwaka. Kwa kukaa bweni wasichana
wataongeza Tsh. 500,000. Jumla ni Tsh 740,000.
V-VI: KUJIANDAA MWAKA MZIMA
KWA MTIHANI WA
KIDATO CHA SITA (History, Kiswahili na Language; au History,
Geography na Kiswahili). Wanaotaka kujiunga wawe wamepata credits
(A, B au C) walau tatu katika masomo yoyote walipofanya au
waliporisiti mtihani wa kidato cha nne. Wawe pia wamepata walau D
katika somo la English. Masomo yataanza tarehe 3-6-2015. Ada ni Tsh.
400,000 kwa mwaka. Kwa kukaa bweni wasichana wataongeza Tsh.
580,000. Jumla ni Tsh 980,000.
MAELEZO MUHIMU KWA WOTE
Ø
Wakristo wa madhehebu yote wanatakiwa kusoma pia Bible Knowledge au
Divinity; kwa wengine ni hiari.
Ø
Ø
Inawezekana pia kupakua fomu kutoka tovuti ya shule halafu kulipa
shuleni Tsh. 20,000 kwa kuigonga mhuri unayoihalalisha. Usikubali
fomu bila mhuri.
Ø
Mbali na fomu, malipo yoyote yanatolewa risiti katika ofisi ya
mhasibu; nje ya hapo malipo si halali, na shule haihusiki nayo, hata
Ø
Ada zote za bweni na zile za masomo ya asubuhi zinaweza kulipwa kwa
mikupuo minne, lakini zile za masomo ya mchana zinatakiwa kulipwa
kwa mkupuo mmoja; zaidi ya ada hakuna mchango unaodaiwa na shule.