Mahali, Majengo na Huduma
Shule inaendelea kujengwa katika manispaa ya Morogoro, kata ya
Kingolwira, mtaa wa Mji Mwema ambao mpaka sasa hauna shule yoyote ya
sekondari.
Katika eneo linalomilikiwa na Jimbo Katoliki la Morogoro, sehemu
inayokusudiwa kutumiwa katika ujenzi wa shule lina ukubwa wa eka
kumi na moja hivi.
Kadiri ya ramani iliyoandaliwa, shule inatarajiwa kufikia idadi ya
ofisi 9, vyumba vya madarasa 31, maabara 2, maktaba 1, ukumbi 1,
nyumba za walimu 6, hosteli kwa wanafunzi 400, bwalo 2, matundu ya
vyoo yasiyopungua 124 n.k.
Mpaka sasa zaidi ya nusu ya majengo hayo imekamilishwa. Kampuni
linaendelea pia kutengeneza samani, pamoja na kununua vitabu na
vifaa vya maabara vya kutosha.
Katika eneo hilo yameingizwa mabomba mengi ya maji safi kwa ajili ya
wanafunzi.
Pia umeme wa Tanesco umeingizwa shuleni. Kwa dharura, lipo jenereta.
Usafiri wa daladala (Mjini-Mikese) unafika karibu na kituo.
Zahanati za binafsi zimejengwa jirani na eneo la shule.